Swahili Internet Governance Glossary

MISAMIATI YA UTAWALA WA MTANDAO


A


ACTA (Anti-Counterfeiting Trade Agreement)
Ni pendekezo la mkataba wa kimataifa uliotiwa sahihi mnamo 2011 kwa ajili ya kubuni sheria za haki miliki.
https://www.eff.org/issues/acta

ADR (Alternative Dispute Resolution)
Ni njia mbadala ya kisheria inayoruhusu wanaozozana haswa kwenye maswala ya mtandao, kusulihisha migogoro nje ya mahakama kupitia mashauriano na maelewano.

AfIGF (Africa IGF)
Ni kongamano la utawala wa mtandao la eneo ya bara Afrika linalofanyika kila mwaka kujadili maswala ibuka yenye umuhimu kwenye mtandao na matumizi yake mfan usalama, ujasusi n.k

AFRINIC (African Network Information Center) 
Ni mojawapo ya mashirika matano ya kimaeneno(RIRs) yenye kutoa rasilimali za mtandao. AFRINIC inawakilisha bara la Africa na ukanda wa bahari ya bara hindi. Shirika la AFRINIC lilianzishwa February 22, 2005 na makao yake makuu ni mji wa Ebene, Mauritius. 
Mkurugenzi mkuu wa AFRINIC ni Alan Barrett kutoka Afrika Kusini.
http://www.afrinic.net/

AFRISIG (African School of Internet Governance)
Ni mradi unaolenga kuwahudumia waandaaji na wazungumzaji wa makongamano ya utawala wa mtandao kimataifa, kimaeneo, na kitaifa kwenye eneo la AFRINIC kupitia kozi za hali ya juu zinazoshughulikia mijadala ya utawala wa mtandao.
Darasa la kwanza la AFRISIG liliandaliwa Durban, Afrika Kusini kutoka 10-12, likiwalenga washiriki 35 kutoka mataifa 15 ya Afrika
 Darasa la pili la AFRISIG liliandaliwa Mauritius kutoka 21-25 Novemba 2014, na kushirikisha washiriki 50 kutoka mataifa 20 ya Afrika
Darasa la tatu la AFRISIG liliandaliwa Addis Ababa, Uhabeshi: 1-5, Septemba 2015. #AfriSIG2015, ilhali la nne

AfTLD (The Africa Top Level Domains Organization) 
afTLD ni ushirikiano wa wasajili wa majina ya ngazi ya juu mtandaoni kwa nchi zilizopo (ccTLD) barani Afrika. Lengo kuu la AfTLD ni kusaidia wasajili wa ccTLD kujadili maswala ibuka yanayoguzia uendeshaji wa ccTLD, na vile vile kutoa msimamo mmoja kuhusu changamoto za mfumo wa majina (DNS) duniani.


AIS (Africa Internet Summit)
Ni kongamano linaloandaliwa kila mwaka na AFRINIC ili kuwaleta pamoja washika dau tofauti tofauti ili kujadili maswala nyeti yenye umuhimu kwa maendeleo ya mtandao barani Africa. Mwaka huu (2016), kongamano hili limefanyika jijini Gaborone, Botswana.



APC (Association for Progressive Communications)
Ni shirika na vile vile mtandao wa kimataifa wa mashirika ya kijamii wenye malengo ya kuwezesha mashirika na watu binafsi kupata huduma nafuu za mtandao kwa ajili ya maendeleo.
APC ina wanachama 50 katika mataifa 35, mengi yayo yakiwa kutoka mataifa yanayoendelea.
APC ilianzishwa mnamo 1990 na inaongozwa na sheria za jimbo la California.
Afisi kuu ya uendeshaji shughuli za APC ipo Johannesburg, Afrika kusini.
http://www.apc.org/

APNIC (Asia-Pacific Network Information Centre) Mojawapo wa mashirika matano ya kimaeneo (RIRs) yenye kutoa rasilmali za mtandao. APNIC inawakilisha bara Asia na eneo la bahari ya kusini 
http://www.apnic.net/

APSIG (Asia Pacific School of Internet Governance)
Ni mradi unaolenga kuwahudumia waandaaji na wazungumzaji wa makongamano ya utawala wa mtandao kimataifa, kimaeneo, na kitaifa kwenye eneo la APNIC kupitia kozi za hali ya juu zinazoshughulikia mijadala ya utawala wa mtandao.

ARIN (American Registry for Internet Numbers)
Mojawapo wa mashirika matano ya kimaeneo (RIRs)yenye kutoa rasilmali za mtandao. ARIN inawakilisha Marekani ya kaskazini (Amerika, Canada, na maeneo ya Karibea na Antarctica).
https://www.arin.net/

ARPANET (Advanced Research Project Networks Agency Network)
Mradi wa utafiti na kimasomo uliotangulia mtandao.
http://computer.howstuffworks.com/arpanet.htm

AT&T
 Shirika la simu na simu ya upepo la Marekani. http://www.att.com/shop/internet/internet-service.html#fbid=5AH6V5gJ_ps • Ni kampuni kubwa ya mawasiliano inayotoa huduma za simu na mtandao.

AUC (Africa Union Commission)
Kamati kuu ya umoja wa Afrika inayotumikia kama tawi kuu au sehemu ya ukatibu katika umoja wa Afrika (AU), mithili na umoja wa ulaya (EU). AUC inajumuisha makamishna wanaoshughulikia sehemu tofauti tofauti za sera. Makao yake makuu ni jijini Addis Ababa, Uhabeshi.

B

DOTBI
.bi ni jina la ngazi ya juu la mtandao kwa nchi ya Burundi. .bi inasimamiwa na Burundi National Center of Information Technology .

Blog (Weblog)
Ni wavuti unaoonyesha taarifa kwa mpangilio wa uchapisho.



BYOD (Bring Your Own Device) Ni mtindo unaozidi kuibuka unaowaruhusu wafanyakazi kubeba vifaa vyao kama vile kipakatalishi (laptop), tabiti (tablets)kwenye sehemu zao za kazi. Hali hii imezua changamoto za kiusalama kwa mashirika haswa kwa data na mitandao ya mashirika.

C

C

CA (Communications Authority)
Ni taasisi ya serikali inayodhibiti shughuli zote zinazohusiana na mawasiliano nchini Kenya). CA iliundwa mnamo 1998, wakati huo ikijulikana kama Communications Commission of Kenya (CCK)
Makao yake makuu ni Westlands, jijini Nairobi.

CC (Creative Commons)
 Ni mfumo wa leseni ya uwazi au huria inayowapa waandishi uhuru wa kugawa au kuachia kazi zao za uandishi kwa umma. 
http://creativecommons.org/

CCWG-Accountability (Cross Community Working Group Accountability)
CCWG-Accountability hukusanya maoni ya jamii na nia ya uboreshaji wa mapendekezo kwa manufaa ya uwajibikaji wa ICANN. Kundi jili limekuwa lenye manufaa sana kwenye mapendekezo ya IANA.



ccTLD (country code Top Level Domain)
Neno lenye nukta mbili zinazoashiria utambulisho wa nchi mtandaoni mfano .ke (Kenya), .tz (Tanzania), zinazoendeshwa na meneja wa nchi husika.
http://www.icann.org/en/resources/cctlds

CERN (European Centre for Nuclear Investigtions)
Ni mradi wa kisayansi wenye makao yake Geneva, Uswisi ambao ulichangia pakubwa kwenye teknohama kupitia uvumbuzi wa WWW na mtandao kwa jumla.
http://home.web.cern.ch/ 



CERT (Computer Emergency Response Team) 
Ni vikundi vya magwiji wa usalama wa teknohama vinavyoundwa kwenye njanja za kitaifa, au kimashirika na malengo ya kuzuia mashambulizi ya kimtandao.
http://www.enisa.europa.eu/activities/cert 



CIPIT (Centre for Intellectual Property in Information Technology)
Ni kituo kilichopo ndani ya chuo cha Strathmore, kinachojihusisha na maswala ya hakimiliki kwenye nyanja ya teknohama, na jinsi haki miliki hizi zinavyoathiri sheria na haki za kibinadamu barani Afrika.
www.cipit.org 


CJEU (Court of Justice of the European Union) 
Mahakama ya haki ya umoja wa nchi za ulaya inayotatua maswala na kuhakikisha sheria zinatekelezwa kote kwenye washirika wa umoja huo.

CoE (Council of Europe) 
Shirikisho la umoja wa ulaya lenye nchi 47 ambazo zinalipa swala la utawala wa mtandao kipa umbele mfano usalama mtandaoni, haki za kibinadamu mtandaoni, ulindaji wa taarifa kuhusu watu na kadhalika.
http://hub.coe.int/ 

COFEK (Consumer Federation of Kenya)
Ni muungano unaotetea haki za watumiaji bidhaa na huduma nchini Kenya.


COP (Child Online Protection) 
Usalama wa watoto mtandaoni kutokana na matishio yanayotakana na mtandao.



CPRSouth (Communication Policy Research South) 
Ni mradi unaojenga uwezo wa kuendeleza wasomi waliopo eneo la Asia na bahari ya kusini, na Afrika kwenye njanja ya sera ya teknohama. 
CPRSouth inalenga haswa wasomi wa kiwango cha chini, na vile vile cha kati.
CPRSouth ilizinduliwa mnamo 2006, huku kongamano lake la kwanza la sera ya teknohama likiandaliwa Januari 2007 jijini Manila, Ufilipino.
Mnamo Aprili 2010, CPRSouth ilizindua mradi wa CPRAfrika, wenye makao yake Cape Town, Afrika Kusini. Mradi huu wa CPRSouth unafadhiliwa na shirika la IDRC la Canada.
Agosti mwaka huu, kongamano la CPRSouth litafanyika kisiwani Zanzibar.

CSCG (Civil Society Coordination Group)
Muungano wa mashirika ya kijamii unaolenga kuafikia na kutoa maamuzi kwa sauti moja.

CSK (Computer Society of Kenya) Ni muungano unaowashirikisha wataalamu wa sekta ya habari, mawasiliano na teknohama nchini Kenya.


CTO (Commonwealth Telecommunications Organisation) Ni shirika la jumuiya ya madola ambalo limepata kuhuduma kwa muda mrefu sana ulimwenguni.
Linajihusisha na maswala ya maendeleo kwenye nyanja ya matumizi ya teknohama kwa ajili ya kujiendeleza kijamii na kiuchumi.
Lilianzishwa mnamo mwaka wa 1901, japo limekuwepo katika hali yake ya sasa ya ushirikano baina ya mataifa tokea 1967. Wanachama wake ni kutoka nchi zilizoendelea sana, zinazoendelea, zilizo na maendeleo duni. 
Makao yake makuu ni London, uingereza

D

DARPANET (Defense Advanced Research Projects Agency) 
Mradi wa idara ya ulinzi ya Marekani ulitangulia mtandao, wakati mwingine ukiitwa ARPANET.
http://searchnetworking.techtarget.com/definition/DARPANET

(DDoS) Distributed Denial Services
 Mpangilio wa mashambulizi unaolenga kuzima mtandao kwa kufutilia mbali huduma muhimu za mtandao.

Diplo (DiploFoundation)
Ni shirika lisilo la kifaida lenye makao yake nchini Malta, na afisi zake jijini Geneva (Uswisi), na Belgrade (Serbia).
Diplo inalenga kuboresha ushirikiano wa washika dau kwenye Nyanja ya diplomasia, uhusiano wa kimataifa, sekta ya sera kama vile utawala wa mtandao, na ubadilikaji wa hela ya hewa.
http://www.diplomacy.edu

DNS (Domain Name System)Mfumo unaoendeshwa na ICANN, unaokubali majina kuongezewa anwani za itifiki mtandaoni (IP).

DNSAFRICA Magazine
Ni jarida linalochapishwa na kampuni ya DNS Africa Communications.
Nakala za jarida hili huguzia mijadala inayohusu ICANN na mfumo wa majina (DNS), barani Afrika na ulimwenguni.

DNSSEC (Domain Name System Security)
Teknolojia ya kiusalama kwenye DNS.
http://www.icann.org/en/about/learning/factsheets/dnssec-qaa-09oct08-en.htm

DoC (Department of Commerce)
Idara ya kiuchumi na biashara ya Marekani. Idara hii ina umuhimu mkubwa kwenye utawala wa mtandao kwa sababu ndio iliyotwikwaa uwezo na mamlaka ya kusimamia shughuli za ICANN.
http://www.commerce.gov/

DoD (Department of Defense) 
Idara ya ulinzi wa Marekani. Idara hii ilijihusisha na na mradi wa DARPANET na kipindi cha mwanzo wa mtandao.
http://www.defense.gov/

dotAfrica (.Africa)
 .Africa ni jina la ngazi ya juu kwenye mtandao lililoidhinishwa na ICANN kwa ajili ya bara la Afrika na jamii zinazoegemea Afrika. .Africa gTLD itahudumu kama jina la eneo la Afrika na eneo la bahari ya bara hindi, na vilevile kwa wale ambao wapo maeneo tofauti nje ya bara.
www.africainonespace.org

E

EAIGF (East Africa IGF) 
Ni kongamano la utawala wa mtandao la eneo ya Afrika mashariki linalofanyika kila mwaka kujadili maswala ibuka yenye umuhimu kwenye mtandao na matumizi yake mfano usalama, ujasusi n.k

EC (European Commission) 
Tume inayowakilisha bara ulaya. Tume hii inajumuisha wahudumu 28 wanaopendekeza na kuhakikisha sheria zinafuatwa na wanachama.
http://ec.europa.eu/ 

E-government (Electronic government)
Inaashiria matumizi ya vifaa vya habari, mawasiliano, na teknohama kuboresha shughuli za utoaji huduma kwa mashirika ya umma.

E-learning (Electronic learning) 
Masomo yanaoendeshwa ki-elektroniki kupitia mtandao.

EuroDIG (European Dialogue on Internet Governance) 
Kongamano la bara ulaya linalojadili maswala ya utawala wa mtandao. EURODIG ilianzishwa 2008 na mashirika tofauti, wawakilishi wa serikali na magwiji ili kuendeleza mjadala na ushirikiano na jamii ya mtandao kuhusu sera za umma kwa ajili ya mtandao. EURODIG huandaliwa kila mwaka kwenye mji mkuu tofauti EuroDIG inafadhiliwa na vikundi vya wafadhili wa mashirika husika, mfano kamati ya Ulaya (Council of Europe –CoE), Umoja wa Ulaya (EU), European Regional At-Large Organization (EURALO), the European Broadcasting Union (EBU),  ICANN, ISOC, the Federal Office of Communications of Switzerland (OFCOM) and the Ré- seaux IP Européens Network Coordination Centre (RIPE NCC). 

http://www.eurodig.org/

Europol (European Police) 
Kitengo cha usalama kinachisaidia mataifa wanachama wa EU kupigana na uhalifu na ugaidi.
https://www.europol.eu/

EUROSSIG (The European Summer School on Internet Governance) Ni shule inayolenga kuwahudumia waandaaji na wazungumzaji wa makongamano ya utawala wa mtandao kimataifa, kimaeneo, na kitaifa kwenye eneo la bara ulaya kupitia kozi za hali ya juu zinazoshughulikia mijadala ya utawala wa mtandao. Tofauti na APSIG na AFRISIG, EUROSSIG inalenga washiriki kutoka mataifa mbali mbali kutoka kote ulimwenguni, huku mataifa yanaoendelea yakipewa kipa umbele.
Masomo ya EUROSIG yanadumu juma nzima na yanafanyika kila mwaka (Julai) jumla ya masaa 48. Kozi hizi zinaguzia mijadala ya utawala wa mtandao kama vile siasa, sheria, uchumi, tamaduni za jamii, ufundi wa teknohama.

F

FBI (Federal Bureau of Investigation) 
FBI ni idara ya ndani ya ujasusi na usalama ya Marekani ambayo inahudumu kama shurika la kudumisha sheria. Inahudumu kwa uelekezi wa idara ya haki.

FCC (The Federal Communications Commission) 
Ni idara huru ya Marekani iliyoundwa na kitengo cha sheria cha bunge la kongres, kudhibiti mawasiliano ya redio, runinga, waya, satelaiti baina ya majimbo, kwenye majimbo yote 50 ya Marekani, wilaya ya Columbia, na maeneo yaliyo chini ya himaya ya Marekani.
 Majukumu ya FCC yanalenga malengo sita yafuatayo: broadband, ushindani, masafa, habari, usalama wa umma, na usalama wa ndani wan chi.
 FCC ilibuniwa na kipengele cha mawasiliano cha mwaka wa 1934, ili kuchukua mahala pa kamati ya taifa ya Redio

FIRE (The Fund for Internet Research and Development) 
Ni mradi wa AFRINIC wa ufadhili unalolenga kusaidia na kukuza ubunifu wenye kutoa suluhu kwa mahitaji ya Afrika, haswa kwenye sekta ya teknohama.
www.fireafrica.org

FOSSFA (Free Software and Open Source Foundation for Africa) 
Ni shirika lisilokuwa la kifaida ambalo lilizinduliwa 2002 na malengo ya kuwaunganisha watu binafsi na mashirika yanayojihusisha na teknohama huria {open source} katika kiwango cha eneo, jimbo na hata nchi. 
Azma ya FOSSFA ni kudumisha utumiaji na utengenezaji wa teknohama huria zinazotoa suluhu na manufaa kwa bara la Afrika. Makao makuu ya FOSSFA yapo mjini Accra, Ghana. www.fossfa.net

G

GAC (Government Advisory Committee) 
Wawakilishi wa serikali mbali mbali, wanaounda kundi la ushauri linaloripoti kwa na kushauri bodi ya ICANN.
https://gacweb.icann.org/display/gacweb/Governmental+Advisory+Committee

GGE (Group of Government Experts) 
Jopo maalum la umoja wa mataifa (UN) ambalo linawajibika kutathmini vitisho vinavyotokana na mazingira ya mtandao, na njia mwafaka wa kushughulikia vitisho kulingana na mustakabali wa sheria za kimataifa.



GIP (Geneva Internet Platform) http://giplatform.org/events Ni mradi wa utawala wa Uswisi unaoendeshwa na DiploFoundation.



GNSO (Generic Name Supporting Organisation) 
Ni ushirika wa wataalamu wanaojihusisha na usajili wa majina mtandaoni.


GSMA (Groupe Speciale Mobile Association) 
GSMA inawakilisha matakwa ya mashirika yanayotoa huduma za simu duniani kote.

gTLD (generic Top Level Domain) 
Majina yaliyofadhiliwa au yasiyofadhiliwa yenye ngazi ya juu kwenye mtandao. Majina ya kwanza 7 yaliyozinduliwa mwaka wa 1980 yalikuwa: .com, .edu, .gov, .mil, .net, .org
http://www.icann.org/en/about/learning/glossary





H HTML (Hypertextt Mark-up Language)
Msimbo au lugha inayotumika sana ketendeneza kurasa za wavuti, na kuandaa taarifa kwa ajili ya maonyesho kwenye wavuti.
http://en.wikipedia.org/wiki/HTML











I IANA (Internet Assigned Names and Authority)
Ni tawi dogo la ICANN linalosambaza rasilmali muhimu za mtandao (IP). IANA inawajibika kugawa rasilmali za IP kwa mashirika matano ya mtandao kimaeneo (RIRs)
http://www.ntia.doc.gov/page/iana-functions-purchase-order ICANN (Internet Corporation for Assigned Names and Numbers)
Shirika lisilo la kifaida lenye makao yake makuu jiji la Los Angeles, California, Marekani.
ICANN inamudu rasilmali za mtandao kwa manufaa ya umma. ICANN inajulikana kwa wadhifa wake kama mwendeshaji wa kiufundi wa mfumo wa majina mtandaoni (Domain Name System).
http://www.icann.org/ ICANN Fellow
Mtu yeyote anayechaguliwa kwenye program ya ICANN Fellowship.

ICANN Fellowship 
Ni ratiba ya ICANN inayofanyika kwenye kila kongamano la ICANN kwa malengo ya kuwawezesha vijana kutoka maeneo mbali mbali ulimwenguni kuwa viongozi wa siku za usoni kwenye nyanja ya utawala wa mtandao.
http://www.icann.org/resources/pages/fellowship-2012-02-25-en ICANNLearn
Ni uga huria na wa wazi unaowezesha jamii ya mtandao duniani kufanya kozi zinazohusiana na mijadala ya ICANN na utawala wa mtandao
http://learn.icann.org/
 ICANNWIKI 
Ni jamii nambari moja yenye rasilmali ya maelezo – watu, vikundi, na mijadala yenye kuvutia ya ICANN na utawala wa mtandao (IG).
http://icannwiki.com 
ICC (International Chamber of Commerce)
Shirika la kushughulikia maswala ya biashara duniani lenye makao yake Paris, Ufaransa.
http://www.iccwbo.org/ 

ICG (IANA Stewardship Transition Coordination Group)
Kundi la kujadili na kuafikia mijadala inayohusu NTIA/ICANN/ na kipindi cha mpwito cha IANA (IANA Transition). ICT (Information and Communication Technology)
Neno linaloelezea matumizi yote ya teknohama. Mbinu na matumizi yake ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi, kulingana na mtazamo wa ITU.
http://en.wikipedia.org/wiki/Information_and_communications_technology 

ICTA (ICT Authority)
Ni tume ya serikali ya Kenya iliyoundwa chini ya idara ya habari, mawasiliano na teknohama ili kusimamia shughuli zinazoambatana na sekta hii. IDN (Internationalised Domain Name)
Majina ya mtandaoni yanayoruhusu nukta zisizo kwenye alfabeti ya kilatini mfano kiarabu, kirusi, kichina.
http://en.wikipedia.org/wiki/Internationalized_domain_name IEEE (Institute of Electrical and Electronics Engineers)
Shirikisho linaloazimia kuendeleza teknohama na ubunifu.
http://www.ieee.org/about/ieee_history.html IETF (Internet Engineering Task Force)
Shirika la kiufundi la mtandao lenye uhusiano na ISOC.
http://www.ietf.org/ IG (Internet Governance)
Utawala wa mtandao, unaozingatia mtazamo wa sheria, jamii, lugha, na uchumi mtandaoni.
http://www.diplomacy.edu/IGBook IG4D (Internet Governance for Development)
Hali ya utumizi wa utawala wa mtandao (IG) kwa ajili ya maendeleo IGC (Internet Governance Caucus) http://igcaucus.org Shirika la kijamii linaloendeleza mijadala mtandaoni ili kutatua maswala yanayohusiana na utawala wa mtandao kama vile haki za kibinadamu, utata wa tamaduni, jamii na maendeleo.
A civil society online discussion group to address Internet governance as it affects human rights, social equity and interdependence, cultural concerns, and social and economic development. IGF (Internet Governance Forum)
Ni kongamano la washika dau linalojadili maswala yanayohusu sera zenye umuhimu kwa mtandao kama inavyobainiwa kwenye mlango wa 72 wa ajenda ya WSIS (Tunis). Mojawapo wa matokeo ya kongamano la WSIS ilikuwa ni kuanzisha kongamano la kimataifa la utawala wa mtandao (IGF), ili kuwezesha washika dau kuchangia kwenye mazingira ambayo yataratibu uundaji wa sera za umma. 
Kongamano la kwanza la IGF liliandaliwa Athens, Ugiriki (2006), kongamano la pili (Rio de Janeiro, Brazil-2007), kongamano la tatu (Hyderabad, India-2008), kongamano la nne (Sharm el Sheikh, Misri-2009), Kongamano la tano (Vilnius,Lithuania-2010), sita (Nairobi, Kenya-2011), saba (Baku, Azerbaija-2012), nane (Bali, Indonesia -2013), tisa (Istanbul, Uturuki -2014), kumi (Joao Pessoa, Brazil -2015).
Mwaka huu kongamalo la kumi na moja litaandaliwa mji wa Guadalajara, nchini Mexico (Disemba).
 http:// www.intgovforum.org IGMENA (Internet Governance for Middle East and North Africa)
Ni kongamano la utawala wa mtandao linalowaunganisha wadau kutoka mashariki ya kati, na kaskazini mwa Afrika kujadili maswala ibuka yanayozungukia utawala wa mtandao (IG) 
IGO (Inter-governmental Organisation)
Shirika lililoundwa kutokana na mkataba baina ya mataifa mawili au zaidi, ili kushirikiana kwenye azma na malenga ya pamoja, haswa amani na usalama.

iHub (Innovation Hub)
iHub ni kitovu cha ubunifu kilichopo jijini Nairobi kwa ajili ya jamii ya teknohama, na uga wa wazi wa wanateknohama, wawekezaji, kampuni za teknohama, na wadukuzi. INTERNET (Interconnected Networks)
Mkusanyiko wa mitandao inayounga tarakilishi na wanaotumia mtandao duniani. 
INTERPOL (International Criminal Police Organisation)
Ni shirika la kimataifa linaloendesha ushirikiano baina ya idara za polisi za mataifa wanachama.
Lina mataifa wanachama 190 na makao yake makuu ni Lyon, Ufaransa.
Rais wa shirika hili ni Mireille Ballestrazzi, na katibu mkuu wake akiwa Jurgen Stock. IoE (Internet of Everything)
Mtandao wa vifaa vyote ni neno linaloashiria uwezo wa kuunganisha kila kifaa kwenye mtandao kwa kutumia IP. IoT (Internet of Things)
Ni neno lilobuniwa na Kevin Ashton mnamo mwaka wa 1999.
IoT ni uwezo wa kutambulisha kila kifaa kilichounganishwa mtandaoni kutumia aina ya kipekee {IP} mfano simu, kipepesi, tabiti, tarakilishi, kamera.

IP (Internet Protocol)
IP ni nambari za kipekee zinazosaidia kwenye kutambua kila kifaa kilichounganishwa kwa mtandao mfano tarakilishi, kipakatalishi, tabiti, kamera, simu, na printa.
Mfumo wa ugawaji wa nambari za IP umepangwa kwa ngazi ya aina yake: Juu kuna IANA – tawi dogo la ICANN, ambalo linagawa rasilmali za IP kwa mashirika matano ya mtandao kimaeneo (RIRs).
RIR zinagawa nambari hizi za IP kwa mashirika ambayo hutenga rasilimali hizi kwa mashirika madogo (LIRs), kampuni, na watu binafsi waliopo chini zaidi ya mpangilio wa ngazi. IPR (Intellectual Property Rights)
Haki miliki kwa mwenye kubuni au kuzindua kitu. IPv4 (Internet Protocol version 4)
Ni aina ya nambari za kipekee zinazotumia anwani yenye nafasi ya biti 32.
IPv4 ilibuniwa miaka ya 1980 na imetumika kwa zaidi ya miaka 30. 
IPV4 ina uwezo wa kumudu anwani bilioni 4.3.
Kati ya hizi anwani 4.3, anwani bilioni 3.7 ndizo zinatumika na vifaa vya kawaida kwenye mtandai. Zilizosalia zinatumika kwenye usambazaji wa anwani spesheli za IP.
Kufuatia kuwa leo hii kuna takribani watu bilioni 3 wanaotumia mtandao, ina maana IPv6 haiwezi kidhii mahitaji ya matumizi kwenye mtandao. IPv6 (Internet Protocol version 6)
Ni aina ya nambari za kipekee zinazotumia anwani yenye nafasi ya biti 128. IPv6 ina anwani trilioni 340 (340 x 10 ^36). Ili kuweza kuelewa kiundani, ulimwengu wa sayari una nyota bilioni, ilhali IPv6 ina anwani trilioni, na trilioni. Hii ina maana kuwa anwani za IPv6 ni nyingi sana kushinda nyota zilizopo kwenye sayari.
Mzunguko wa dunia kwa jua ni mkubwa kiasi kwamba unaweza kubeba dunia zingine 3,262. Hii ina maana inaweza kuchukua dunia nyingine trilioni 21,587,961,064,546 (kama hii tuliyomo) kuweza kumaliza kabisa anwani zote za IPv6.

ISOC (Internet Society)
Ni shirika la kimataifa, lisilo la kifaida ambalo lilizinduliwa mwaka 1992 na Vint Cerf – mvumbuzi wa TCP/IP, na lengo la kutoa mwongozo kwenye maswala yanayohusiana na (standards) mtandao, elimu, matumizi, na sera.
Maono yake ni kuendeleza uwazi, mabadiliko na matumizi ya mtandao kwa manufaa ya watu wote ulimwenguni.

ISOC inajumuisha vitengo kama vile Internet Engineering Task Force (IETF), Internet Architecture Board (IAB), Internet Engineering Steering Group (IESG), na Internet Research Task Force (IRTF). Makao makuu ya ISOC yapo Reston, Virginia, Marekani (karibu na Washington, D.C.), afisi zake zipo Geneva, Uswisi. ISOC ina uanachama wa zaidi ya mashirika 140, na wanachama wa 80,000 wa kibinafsi.
Wanachama pia huunda makundi (chapters)kulingana na kanda walizomo au uraibu wao. Kuna makundi (chapters) zaidi ya 110 ulimwenguni.
http://www.internetsociety.orgISP (Internet Service Provider)
Shirikia (haswa la kibiashara) linalotoa huduma za kuunganisha watu kwenye mtandao. IT (Informationa Technology)
Matumizi ya vifaa vya teknohama kuweka data, kutoa, kutuma na kadhalika.
 ITR (International Telecommunications Regulations)
Mkataba uliowekwa mwaka wa 1988 kuwezesha uunganishwaji na utenda kazi baina ya vifaa vya mawasiliano. Mkataba huu ulirekebishwa kwenye kongamano la WCIT lililofanyika Dubai mwaka wa 2012 baada upigaji kura uliozua utata.
http://www.internetsociety.org/itr ITU (International Telecommunication Union)
Shirika mmoja wapo la umoja wa mataifa lenye makao yake Geneva, Uswisi. Linajihusisha na maswala ya habari na mawasiliano.
http://www.itu.int/en/Pages/default.aspx IXP (Internet Exchange Point)
Ni muundo mbinu ambao unaruhusu kubadilishana kwa mawasiliano baina ya mitandao tofauti, haswa kupitia maelewano


K KB (Kilobyte)
Kipimo cha uwezo wa data. KB 1 ni sawa na bytes 1024. Vile vile, MB inasimamia Megabyte na inaashiria kilobytes elfu (sawa na bytes milioni); GB inasimamia Gigabyte na inaashiria maelefu ya Megabytes (bytes bilioni) Kbps (Kilobits per second)
Kipimo cha mwendo wa uhamisho wa data.

.KE (dot KE)
.ke ni utambulisho wa nchi ya Kenya (ccTLD)kwenye mtandao.
.ke ilikabidhiwa kwenye Root Zone mnamo Aprili 1993. 
Daktari Shem Ochuodho (usimamizi) na Randy Bush (ufundi) walikuwa wahudumu wa kujitolea kusimamia maswala ya .ke.
Karibia mwaka wa 2000, jamii ya washika dau, wa umma na kibinafsi, waliafikiana na kuunda shirika lisilokuwa ka kifaida kwa ajili ya kusimamia maswala ya .ke.
.ke inajivunia takribani sajili 60,000 hadi sasa, na imeiga mfumo wa usajili {registry/registrar). Usajili mwingi unatekelezwa na kampuni zilizopo nchini Kenya.

KENIC (Kenya Network Information Centre)
Shirika lisilo ka kifaida ambalo linasimamia shughuli za .ke.
www.kenic.or.ke 


KESIG (Kenya School of Internet Governance)
Ni mradi unaolenga kuwahudumia waandaaji na wazungumzaji wa makongamano ya utawala wa mtandao (IG) kimataifa, kimaeneo, kitaifa nchini Kenya kupitia kozi za hali ya juu zinazoshughulikia mijadala ya utawala wa mtandao. Shule hii ilizinduliwa rasmi Julai 2016 kwa ufadhili wa HIVOS.

 KICTANET (The Kenya ICT Action Network)

Ni uga wa washika dau, watu, mashirika yenye uvutio wa kujihusisha na sera za teknohama, na udhibiti. Mtandao huu unalenga kusisimua mabadiliko kwenye sekta ya teknohama, kwenye juhudi za kuunga mkono lengo la taifa la teknohama la kuwezesha ukuzaji na maendeleo.
http:// www.kictanet.or.ke

KIGF (Kenya Internet Governance Forum)
Ni kongamano la washika dau mbali mbali linaloandaliwa kila mwaka nchini Kenya, na linalenga kuwakutanisha wadau kujadili maswala yanayohusu sera zenye umuhimu kwa mtandao kama inavyobainiwa kwenye mlango wa 72 wa ajenda ya WSIS (Tunis).
http://www.kenyaigf.or.ke KIXP (Kenya Internet Exchange Point)
Ni kituo kinachoruhusu ubadilishana wa mawasiliano baina ya mitandao tofauti nchini Kenya bila ya kuyaelekeza kwenye mitandao mingine ya kimataifa.
 L LACNIC (Latin America and Caribbean Network Information Centre)
Ni shirika linalosimamia ugavi wa rasilmali muhimu za mtandao eneo la Marekani ya kusini, na sehemu za karibea.
http://www.lacnic.net/web/portal/inicio

LIR (Local Internet Registry)
Mashirika yanayojihusisha na usambazaji wa anwani za mtandaoni na usajili wa rasilimali ndani ya nchi husika.




M MAG (Multi-stakeholder Advisory Group) 
Ni jopo linalowajibika kuandaa kongamano la IGF kila mwaka.
Kando na kongamano kuu la IGF, kuna makongamano ya kitaifa (local IGF), kimaeneo (regional IGF) mfano EAIGF, WAIGF, SAIGF, na AfIGF. MDGs (Millenium Development Goals)
Malengo ya maendeleo ya millennia
http://www.un.org/millenniumgoals/ 
Makubaliano ya mataifa wanacjama wa umoha wa mataifa (UN) kushirikiana kutimiza malengo nane ili kuafikia matakwa ya masikini. Mbps (Megabits per seconds)
Kipimo cha mwendo wa uhamisho wa data; megabit kwa sekunde au bits milioni kwa sekunde (Mbps).
 MILNET (Military Network)
Sehemu ya ARPANET iliyotumika na idara ua ulinzi ya Marekani (DoD).
http://en.wikipedia.org/wiki/MILNET MIT (Massachusetts Institute of Technology)
Chuo kilichoanzishwa mwaka wa 1861 katika jimbo la Massachusetts, Marekani, kwa ajili ya usomi wa sayansi na teknolojia.
http://web.mit.edu/ MODEM (Modulate-Demodulate)
Kifaa kinachotumiwa kutuma na kupokea data ya kidijitali.
 MOOCS (Massive Open Online Courses)
Ni kozi huria za mtandaoni zinalenga washiriki wengi. Kando na kozi za kawaida, kozi hizi zinajumuisha video kutoa masomo kwa washiriki.

MoU (Memorandum of Understanding)
Mkubaliano wa maelewano unaotoa taarifa za kina kwenye mkataba baina ya pande husika, hujumuisha matakwa na majukumu ya wahusika. Kwenye Nyanja za utawala wa mtandao, neon hili linatumiwa kuashiria makubaliano baina ya ICANN na idara ya kibiashara ya Marekani (DoC) MP3 (Motion Picture Experts Group, Audio Layer 3)
Ni faili endelezi kwa faili ya MP3. MSP (Multistakeholder Process) http://toronto45.icann.org/node/34391 Ni mbinu ya kuwezesha maelewano baina ya washika dau wenye maoni tofauti kutoka kwenye umma, serikali, sekta ya kibinafsi, na mashirika ya kijamii.













N NCSG (Non Commercial Stakeholder Group)
Ni muungano wa mashirika yasiyo ya kifaida ndani ya ICANN GNSO.
NCSG ina uwezo kamili wa kupiga kura ndani ya ICANN, na inaunda na kuunga sera zinazolinda mawasiliano au shuhguli zisizo zaa kibiashara/kifaida mtandaoni.
NCSG pia inajihusisha kwenye uteuzi wa wanabodi wa ICANN. 
NCUC (Non Commercial User Constituency)
Ni shirika linalounganisha watu binafsi na mashirika mengine ya kijamii, au yasiyo ya kifaida kwenye uundaji wa sera ndani ya ICANN. Shirika hili lina uwezo wa kupiga kura halisia.
NCUC ina wanachama 505 kutoka mataifa 134, miongoni mwao yakiwemo mashirika 117 yasiyokuwa ya kifaida, huku 388 wakiwa wanachama binafsi.
Shirika hili linaongozwa na mwenyeketi (Rafik Dammak), Mwanakamati mkuu APNIC (Zuan Zhang), Mwanakamati mkuu LACNIC (Joao Caribe), Mwanakamati mkuu ARIN (Milton Mueller), Mwanakamati mkuu RIPE NCC (Farzaneh Badii), Mwanakamati mkuu Africa (Grace Githaiga) NIC (Network Information Centre)
Inaashiria mashirika matano ya kimaeneo (RIRs) yanayojihusisha na ugavi wa rasilmali muhimu za mtandao (IP). Mashirika hayo ni AFRINIC, APNIC, ARIN, LACNIC, na RIPE NCC.

NIST (National Institute of Standards and Technology)
Asisi hii ilianzishwa mnamo 1901 kama kituo cha utafiti cha serikali ya Marekani. NIST inajihusisha na upimaji wa uafikiaji wa viwango kwenye sayansi. Hivi karibuni, NIST imekuwa mstari wa mbele kwenye usalama wa mtandao, na vile vile ulindaji wa mtandao.

NoMCom (The Nominating Committee) 
NomCom ni kamati huru iliyo na jukumu la kuwachagua wanachama nane wa bodi ya wakurugenzi na nyadhifa zingenezi ndani ya ngazi ya ICANN kama ilivyopitishwa kwenye sheria ndogo za ICANN NPOC (Not for Profit organizational Concerns)
Ni mojawapo wa mashirika yanayojihusisha na shughuli za mashirikia yasiyo ya kifaida ndani ya ICANN.
Ilitambuliwa rasmi na bodi ya ICANN mnamo Juni 24 2011 wakati wa kongamano la ICANN la 41, Singapore.
NPOC inajihusisha haswa na sera zinazoathiri DNS. NPOC inalenga kuyapa mashirika yasiyokuwa ya kifaida sauti, na uwazi kwenye utoaji wa habari. NRO (Number Resource Organisation)
Inajumuisha mashirika matano ya kimaeneo (RIRs) kwenye juhudi zao za kushirikiana katika ugavi, na ulinzi wa rasilmali, pamoja na uundaji wa sera kwa pamoja.
 NSF (National Science Foundation)
Ni kitengo huru cha serikali kilichoundwa na bunge la Kongres mnamo 1950 ili kuendeleza sayansi; kufanikisha afya ya kitaifa, na usalama wa taifa.
http://www.nsf.gov/ NSFNET (National Science Foundation Network)
Mradi wa kompyuta uliozinduliwa 1984, ili kuwezesha utendaji kazi wa hali ya juu wa watafiti kote nchini (Marekani).
http://www.nsf.gov/about/history/nsf0050/internet/launch.htm NTIA (National Telecommunications and Information Administration)
Ni shirika na mshauri mkuu wa rais wa Marekani kwenye maswala yanayohusu sera za mawasiliano na habari. Ni mojawapo wa nguzo muhimu kwenye mkataba baina ya serikali ya Marekani na ICANN.
http://www.ntia.doc.gov/about






O ODR (Online Dispute Resolution)
Njia mbadala ya kusuluhisha mizozo mtandaoni. Ni sawa na ADR; inatumia teknolojia kutatua malumbano baina ya washirika. OECD (Organisation of Economic Co-operation and Development)
Shirika lenye makao yake makuu Paris, Ufaransa ambalo linaafikia kutoa ukumbi ambao mataifa yanaweza kushirikiana kwa pamoja kutatua matatizo. OERs (Open Educational Resources)
Ni rasilimali zozote za masomo zilizopo mtandaoni zinazolenga matumizi kwa umma. Leseni ya rasilimali hizi ni huria kana kwamba yeyote anaweza kuzitumia kisheria kwa kuziiga, kuzinakili, na kuzisambaza bila pingamizi, mradi amezingatia vigeo vya leseni.

OGP (The Open Government Partnership)
OGP ni mradi wa wazi wa utawala, na wa ushirikiano unaolenga kutimiza uwajibikaji kutoka kwa serikali ili kuboresha uwazi, kuwezesha wananchi, kupigana na rushwa, na kuiga mbuni mpya za teknohama kwa ajili ya kuongeza thamani na nguvu kwenye utawala.
 OSI (Open Standards Interconnection)
Ni shirika la ubora wa bidhaa kwa vifaa vya mawasiliano duniani Open Technology Fund (OTF)
Ni shirika lisilo la kifaida lenye makao yake makuu Washignton D.C ambalo azma yake ni kusaidia miradi inayolenga uhuru wa mtandao ili kuwawezesha watu kupata huduma za uwazi mtandaoni bila pingamizi. OTT (Over-the-top)
Msamiati unaotumiwa kuashiria huduma zinazotolewa mtandaoni bila ya kushirikisha watoa huduma wa mtandao mfano Skype, Google, Facebook, Twitter)



P PC (Personal Computer)
Tarakilishi au kompyuta inayolengwa kwa matumizi ya kibinafsi. PDP (Policy Development Process)
Inaashiria hali ya uundaji sera zinazochangia mwelekeo wa utawala wa mtandao na matumizi yake PGP (Prety Good Privacy)
Programu maarufu inayotumiwa kusimba au kusimbua barua pepe mtandaoni. PKI (Public Key Infrastructure)
Mkusanyiko wa maunzi, program, watu, sera, na mbinu zinazohitajika kutengeneza, kusimamia, kusambaza, kutumia, kuhifadhi, na kutengua vyeti vya kidijitali.
http://en.wikipedia.org/wiki/Public-key_infrastructure PRISM
Programu ya kisiri inayotumiwa na idara ya usalama ya Marekani (NSA), kukusanya mawasiliano yanayofanyika kwenye mtandao.
Mpango huu wa kisiri ulizinduliwa mnamo mwaka wa 2007 na serikali ya George W. Bush.
 PS (Packet Switching)
Ni mbinu inayotumia itifaki za mtandao wa kompyuta kuwasilisha data kwenye mwishilio.
http://compnetworking.about.com/od/networkprotocols/f/packet-switch.htm





R

RDS (Registry Directory Services)
Ni hifadhi ya mtandaoni iliyopendekezwa kuchukua pahali pa WHOIS. RFC (Request for Comments)
Inatumiwa kuashiria machapisho ya IETF. Machapisho haya yalizinduliwa mwaka wa 1969 na Steve Crocker, mwanabodi wa sasa wa ICANN, kunakili matukio ya ARPANET. Siku hizi yanatumiwa kunakili mapendekezo ya mwelekeo wa mtandao, na itifaki za mawasiliano. RIPE NCC (Réseaux IP Européens Network) Ni mojawapo wa mashirika matano ya kimaeneo (RIRs), linalosimamia ugavi wa rasilmali muhimu za mtandao (IP) eneo la bara ulaya. RIR (Regional Internet Registry)
Mashirika yasiyo ya kifaida ambayo yanasimamia na kuendesha shughuli za ugavi wa rasilmali za mtandao (IP). Kuna mashirika 5: AFRINIC, APNIC, ARIN, LACNIC, na RIPE NCC. Mashirika haya hufanya kazi kwenye miradi kwa pamoja.

RSSAC (Root Server System Advisory Committee) RSSAC inawajibika na utoaji ushauri kwa jamii ya ICANN, na wanabodi kuhusu maswala yanayoguzia oparesheni, usimamizi, usalama,na hadhi ya mfumo wa Root Server (Root Server System), kama ilivyo kwenye mwongozo wa sheria ndogo za ICANN.
 RTC (Real Time Chat)
Ni uwezo wa kupokea jumbe kwenye mtandao kwa wakati mwafaka, pindi zinapotumwa.
 .RW (DOTRW)
.rw ni ni jila la usajili la ngazi ya juu mtandaoni kwa nchi ya Rwanda
.rw ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1996.


S

SSAC (Security and Stability Advisory Committee)
Ni kamati inayoshauri jamii ya ICANN na wanabodi kuhusu maswala ya usalama na hadhi ya mfumo wa mtandao wa majina na anwani (naming and address allocation systems). SAIGF
Ni kongamano la utawala wa mtandao la eneo ya Afrika ya kusini linalofanyika kila mwaka kujadili maswala ibuka yenye umuhimu kwenye mtandao na matumizi yake mfano usalama, ujasusi n.k

SEACOM
Ni kampuni inayoendesha mitandao ya nyaya za mawasiliano baharini na zile za nchi kavu za mkonga (fibre-optic) zenye mwendo kasi, zinazohudumia pwani za Afrika mashariki na Magharibi. SDGs (Sustainable Development Goals)
Malengo yaliyokubaliwa na wanachama wa umoja wa mataifa (UN), yanayoguzia maswala mengi mengi ya maendeleo. SOPA (Stop Online Piracy Act)
Mswada pendekezo unaowalenga tovuti zenye kukiuka haki miliki na kazi za wasanii
 Spam Linatokana na neno SPAM (Hormel Spiced Ham) http://en.wikipedia.org/wiki/Spam_%28electronic%29 
Ni utumaji wa jumbe taka za kielektroniki kwa jumla, kwa ajili ya matangazo pasi na kubagua.

SRI (Stanford Research Institute) http://www.sri.com/about Shirika lisilokuwa la kifaida ambalo linajihusisha haswa na utafiti uliofadhiliwa na serikali, nyakfu, na mashirika mengine.
Kwa sasa linajulikana kama SRI International SSL (Secure Sockets Layer) 
Safu ya usalama bora kwenye teknohama inayotumiwa kubainisha kiungo kilich salama kati ya sava mtandaoni (web server) na kivinjari (browser). 
Kiungo hiki kinahakikisha data zinazopitia kati ya sava na kivinjari zinabakia kuwa za siri.
SSL ni kiwango kinachotumiwa na mamilioni ya mitandao kulinda malipo ya mitandaoni kwa wateja wao.
http://www.digicert.com/ssl.htm












T

TESPOK (Technology Service Providers of Kenya)
TESPOK ni shirika la kitaalamu, lisilo la kifaida ambalo linawakilisha maslahi ya wanaotoa huduma za teknohama nchini Kenya. TESPOK lilianzishwa mnamo 1999, na nguvu za muungano huu zipo ndani ya uwezo wake wa kuwakilisha sekta hii kwa jumla.
Ruwaza ya TESPOK ni “kuwa kiongozi wa ukuaji na ubora wa teknohama barani Afrika”.

TCP/IP (Transmission Control Protocol/Internet Protocol)
TCP/IP ni kitengo chenye umuhimu mkubwa sana kwenye mtandao. 
Viwango vya TCP/IP vinawekwa na shirika la IETF.
Kutokana na umuhimu wake, TCP/IP ni mojawapo wa kiwango kinachopewa umakinifu wa hali ya juu kwenye mtandao na shirika la IETF.

TCRA (Tanzania Communications Regulatory Authority) Ni asisi ya serikali inayodhibiti shughuli zote zinazohusiana na mawasiliano nchini Tanzania. Asisi hii iliundwa mnamo 2003 ili kusimamia mawasiliano ya ki-elektroniki, huduma za Posta, na usimamizi wa wigo wa kitaifa wa urushaji mawimbi. Asisi hii ilianza majukumu yake rasmi mnamo tarehe 1 Novemba 2003, na kuchukua pahala pa iliyokuwa tume ya mawasiliano Tanzania(TTC) na tume ya Utangazaji (TBC) Makao makuu ya asisi hii ni jijini Dar es Salaam.

TLD (Top Level Domain)
Mfumo wa mtandao wa DNS unawawezesha watu kufikia kurasa na rasilmali zinginezo kwa kutumia majina ambayo ni rahisi kukumbuka mfano www.icann.org badala ya kutumia anwani ya IP kama 192.0.34.65.
Kila jina (domain name) linaundwa na mkurupuko wa maneno madogo (yanaoitwa labels) ambayo yanatenganishwa na .(dot).
Neno lililopo kulia mwa jina linafahamika kama top-level dmain (TLD). ToS (Terms of Service)
Makubaliano ya huduma, au sheria na vigezo ambavyo anayepania kutumia huduma fulani mtandaoni anahitaji kusoma, na kukubali kama sehemu ya mkataba wa makubaliano kabla ya kutumia huduma hiyo.


TRIPS (Trade Related Aspects of Intellectual Property Rights) http://www.wto.org/english/thewto_e/whatis_e/tif_e/agrm7_e.htm 
Ni sheria zinazohusiana na haki miliki zilizotokana na mkataba wa WTO. TTIP (Transatlantic Trade and Investment Partnership)
Ni mkataba huria wa biashara na uwekezaji baina ya Marekani na umoja wa Ulaya (EU). Mkataba huu umeweza kufutiliwa mbali na rais Donald Trump pindi tu alipoingia madarakani. .TZ (DOTTz)
Ni jina la ngazi ya juu mtandaoni kwa nchi ya Tanzania lililozinduliwa mnamo 1995.
Msajili wa .tz ni tzNIC, ilhali mfadhili mkuu wake ni chuo kikuu ya Dar es Salaam. TzNIC (Tanzania Network Information Center) Ni shirika Iisilo la kifaida lililobuniwa na tume ya mawasiliano ya Tanzania (TCRA) ili kuendesha oparesheni na usajili wa jina la ngazi ya juu la nchi mtandaoni (.tz). TzNIC iliundwa mnamo 16 Novemba, 2006. Kufikia sasa, TzNIC ina sajili za .tz karibia 12,000. Hivi majuzi, tume ya TCRA ilitoa makataa kwa kampuni zote nchini Tanzania kusajili na .tz


U UCLA (University of California, Los Angeles)
Chuo cha umma cha utafiti kilichoko Los Angeles, CA, Marakani.
http://www.ucla.edu/ UCSB (University of California, Santa Barbara)
Chuo cha umma Santa Barbara, CA, Marekani http://www.ucsb.edu UDHR (Universal Declaration of Human Rights)
Mkataba wa haki msingi za kibinadamu wa umoja wa mataifa kama ulivyopitishwa na baraza kuu la umoja huo, UNGA, mwaka wa 1948.
http://www.un.org/en/documents/udhr/ UDRP (Uniform Domain-Name Dispute-Resolution Policy)
Sera ambapo utata wa nembo za biashara (trade marks) zinazohusiana na mtandao wafaa kutatuliwa kwa makubaliano, uamuzi wa mahakama, wahusika kabla ya msajili (registrar) kufutilia mbali, kuhamisha kinachozozaniwa.
http://www.icann.org/en/help/dndr/udrp 

.UG (DOTUG)
Ni usajili wa ngazi ya juu mtandaoni wan chi ya Uganda.
.ug ilianzishwa mnamo mwaka wa 1995.

UN (United Nations)
Shirika la umoja wa mataifa lenye wanachama 193, lililobuniwa mnamo 1945 kuchukua pahala pa ligi ya mataifa (League of Nations).
http://www.un.org/en/ 

UNCITRAL (United Nations Commission on International Trade Law)
Kitengo kikuu cha cha Umoja wa Mataifa (UN) kwenye uga wa kimataifa wa sheria za kibiashara
http://www.uncitral.org/

UNDESA (United Nations Department of Economic and Social Affairs)
Ni sehemu ya ukatibu wa Umoja wa Mataifa (UN Secretariat) ambayo inawajibika kufuatilia makongamano au mikutano mikuu ya Umoja wa Mataifa. UNDESA inasaidia mataifa kuweka ajenda na maamuzi kwa malengo ya kusaidia kutimiza changamoto za kiuchumi, kijamii na mazingira.
 UNDESA iliundwa mnamo 1948, na makao yake makuu ni jijini New York, Marekani. Kiongizi wa sasa wa UNDESA ni Wu Hongbo.
http://www.un.org/development/desa/en 
 UNESCO (United Nations Educational Scientific and Cultural Organization)
Kitengo maalum cha Umoja wa Mataifa (UN) chenye program tano kuu: elimu, sayansi ya mazingira, sayansi ya jamii, utamaduni, mawasiliani na habari.
https://en.unesco.org/ 

UNGA (United Nations General Assembly)
Baraza kuu la umoja wa mataifa.

UNICEF (United Nations Children’s Education Fund) http://www.unicef.org/ 
Ni program ya Umoja wa Mataifa (UN) inayotoa huduma za kibinadamu na misaada kwa watoto. UNICEF ni mshika dau mkuu kwenye ulindaji wa watoto mtandaoni (COP). UNIX
Ni aina ya uendeshaji mfumo (OS) unaotumia miito ya mstari amri (command line). 
 V VoIP (Voice over Internet Protocol)
Njia ya nafuu ya maongezi ya sauti kupitia mtandao.










W WAIGF (West Africa Internet Governance Forum)
Ni kongamano la utawala wa mtandao la eneo ya Afrika ya magharibi linalofanyika kila mwaka kujadili maswala ibuka yenye umuhimu kwenye mtandao na matumizi yake mfano usalama, ujasusi n.k W3C(World Wide Web Consortium)
Jamii ya kimataifa yenye wanachama na wafanyakazi wanaohuduma kuunda sera zenye kulenga ubora kwenye mtandao.Jamii hii inaongozwa na mvumbuzi wa WWW Tim Berners-lee na mkurugenzi mkuu Jeffrey Jaffe.
Ruwaza ya Wc3 ni kuongoza mtandao kwa uwezo wake kamili.
 WCIT (World Conference on International Telecommunications) http://www.itu.int/en/wcit-12/Pages/default.aspx 

WGIG (Working Group on Internet Governance)
Tume iliyobuniwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya hatua kuhusu utawala wa mtandao (Internet Governance).

WHOIS 
Hifadhi iliyo wazi kwa umma inayoonyesha taarifa za mashirika, na vile vile watu binafsi. Taarifa za hifadhi hii zinahusiana na usajili wa rasilimali za mtandao kama vile nambari za kipekee (IP), na majina (Domain Names)

WIPO (World Intellectual Property Organisation)
Kitengo cha umoja wa mataifa (UN) ambacho kinahusika haswa na maswala ya haki miliki kama njia moja ya kukuza ubunifu. WIPO iliundwa 1967 “kuwezesha ubunifu, na kuendeleza ulindwaji wa haki miliki kote duniani. WIPO ina mataifa wanachama 188, nainasimamia mikataba 26 ya kimataifa. Makao yake makuu ni Genevea, Uswisi.
Mkurugenzi mkuu wa sasa wa WIPO ni Francis Gurry, ambaye alitwaa uongozi Octoba1, 2008. Mataifa yasiyo wanachama wa WIPO ni visiwa vya Marshall, Mkusanyiko wa visiwa vya Micronesia, Nauru, Palau, Visiwa vya Solomon, Sudan Kusini, Timor-Mashariki, Palestina na yana hadhi ya utazamaji tu

WITSA (World Information Technology And Services Alliance)
Ni muungano ulioanzishwa kwa ajili ya kuwaunganisha wanachama waliopo kwenye sekta ya teknohama katika mataifa mbali mbali.

WSIS (World Summit on Information Society)
Kongamano lililofanyika kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ilifanyika Geneva, Uswisi tarehe 10 hadi 12 Disemba 2003; awamu ya pili ilifanyika Tunis, Tunisia kutoka tarehe 16 hadi 18 Novemba 2005. WSIS+10
WSIS ilisherehekea miaka 10 tangu kongamano la Tunis (2005). Kwenye kongamano la Tunis, kulikuwepo na maelewano kuwa utawala wa mtandao (IG) udhihirishe uhalisia wa washika dau wote (multi-stakeholders).
Kuendelea ushirikiano ilikuwa mbinu ya aina yake iliyolenga uundaji wa mstakabali mpya wa wahishika dau wote (multi-stakeholders) katika utawala.
Miaka 10 tangu matukio ya WSIS, washika dau husika (RIRs, mataifa, mashirika ya kijamii, wanasheria walijihusisha kwenye kuchunguza matokeo yake ndani ya muongo huo. Matokeo haya yaliwakilishwa kwenye kongamano la umoja wa mataifa (UNGA), jijini New York , Disemba 2015.

WTO (World Trade Organisation)
Shirika la kimataifa linaloendeshwa na mataifa wanachama, ambalo linalenga kupanua hali ya biashara kwa manufaa ya wote.
WTO ilianzishwa Januari 1 1995 chini ya mktaba wa Marrakesh. Ilitiwa sahihi na mataifa 123 Aprili 15 1994, na kuchukua mahala pa General Agreement on Tariffs and Trade (GATT), ambayo ilianzishwa 1948. WTO inatoa mwongozo wa mikataba baina ya mataifa husika, na vile vile kusaidia kutatua mizozo

WWW (World Wide Web)
Ni mfumo ambao umeunganishwa kwa njia ya msimbo (HTML) ambao unatuwezesha kufikia kurasa za wavuti kwenye mtandao.




X XML (eXtensible Mark-up Language)
Msimbo ulioigwa kutoka SGML (ISO 8879).











YCIG (The Youth Coalition on Internet Governance)
YCIG ni uga ulio wazi kwa chipukizi na vijana wote waliopo chini ya miaka 30 ambao wanavutiwa na maswala ibuka ya utawala wa mtandao.












Z ZACR (ZA Central Registry) 
Shirika lisilo la kifaida lililozinduliwa 1988 kusimamia usajili wa jina la ngazi ya juu mtandaoni (ccTLD) nchini Africa kusini. Hapo awali, ZACR ilijulikana kama UniForum SA. Kufikia 2016, ZACR inajivunia wasajili zaidi ya milioni 1 wa .za