Portal:Internet Governance

From ICANNWiki
Revision as of 19:06, 27 June 2016 by Jacob Iteba (talk | contribs)
Jump to navigation Jump to search

Linkedin

Ni mtandao wa kijamii. Tofauti na mitandao mingine ya kijamii, LinkedIn ina muegemeo wa kibiashara ambao unalenga kuwaunganisha waajiri au waajiriwa na mitandao mingine ya watu. Mtandao huu ulianzishwa Disemba 14 2002 na kufikia sasa una watumiaji milioni 400. Makao yake makuu ni Mountain View, California, Marekani. Hivi Karibuni, kampuni ya Microsoft imetangaza kukamilisha harakati za ununuzi wa LinkedIn kwa kitita cha $26.2 bilioni.

Dropbox

Mtandao unaowezesha watu kuhifadhi picha, nakala, video, na faili zingine kwa ajili ya urahisi wa usambazaji. Dropbox ilianzishwa 2007 (Juni, 2007), na makao makuu ya Dropbox ni San Francisco, California.

Wiki

Wiki ni jina linalotokana na neon “wiki wiki” ambalo lina ashiria “haraka” kwenye lugha ya Hawaii.

Wiki ni kitengo cha mtandao kinachowezesha jamii ya watu kushirikiana na kuchangia maelezo na mijadala mbali mbali yenye mada ya kuvutia.

Wikileaks

Ni hifadhi na pia shirika la kimataifa la habari lililoundwa na Julian Assange 2006. Wikileaks inajihusisha na utoaji wa taarifa nyeti, za siri zinazohusiana na ufisadi, ujasusi, vita na kadhalika.